
Klabu ya soka ya Liverpool imeunza
mwaka mpya wa 2016 vibaya baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa
wagonga nyundo wa London klabu ya West Ham.

Mabao
ya West Ham yalipachikwa kimiani na wachezaji wake Michail Antonio na Andy
Carroll katika dimba la uwanja wa Upton Park.
Sasa
Liverpool imesalia katika nafasi ya 8 ikiwa na pointi zake 30 huku west Ham
wakipanda hadi nafasi ya 5 wakikunja kitita cha pointi 32.
Post a Comment