
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
nchini (TFF), Jamal Malinzi amempongeza mshambuliaji wa timu ya Taifa ya
Tanzania “Taifa Stars” Mbwana Samatta kwa kufanikiwa kujiunga na klabu ya Genk inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini Ubeligiji.
Malinzi amempongeza Samatta kwa
kupata nafasi ya kucheza ligi kuu ya Ubeligiji baada ya kusaini mkataba wa
miaka mitatu na nusu kuichezea RC Genk inayoshika nafasi ya sita kwenye msimamo
wa Ligi Kuu nchini humo.
Kufuatia kupata nafasi hiyo, Malinzi
amemtaka Samatta kujituma kwa nguvu zake zote na uwezo wake wote ili kuendelea
kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania katika nyanja za kimataifa na kwa sasa
barani Ulaya.
Aidha
Malinzi amewataka wachezaji wengine kujituma na kutumia nafasi wanazozipata
katika vilabu vyao kwa kufanya vizuri na kupata nafasi ya kuvuka kwenda kucheza
soka la kimataifa nchi za nje.
Post a Comment