
Klabu ya Manchester United usiku wa jana wameamka
usingizini baada ya kuichapa klabu ya Derby mabao 3-1 katika raundi ya nne ya
Kombe la FA.
Wayne Rooney alifunga kwa kombora alilolitoa akiwa
hatua 20 kutoka golini mwa wapinzani wao na kuwaweka United mbele dakika ya 16
kabla ya George Thorne kupenya safu ya ulinzi ya vijana hao wa Van Gaal na
kusawazisha dakika ya 37.
Kipindi cha pili Daley Blind aliwarejesha mbele baada
ya kupokea krosi kutoka kwa Jesse Lingard dakika ya 65.
Juan Mata alikamilisha ushindi wao wa mabao hayo 3
katika dakika ya 83 ya mchezo na kuifanya itoke vifua mbele siku ya jana.
Derby, ambao hawajashinda mechi yoyote katika ligi yao
mwaka 2016 wanashikilia nafasi ya tano katika ligi ya Championship.
Post a Comment