
Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Tanzania Mbwana
Ally Samatta maarufu kama Samagoal hatimaye leo hii amesaini mkataba wa miaka 4
na klabu yake mpya ya Genk nchini Ubelgiji.
Akizungumza na KILOWOKO.BLOGSPOT.COM
baba mzazi wa Mnwana Mzee Ally Samatta amesema mtoto wake huyo amesaini mkataba
wa miaka minne na klabu yake hiyo mpya lakini anachokisubiri kwa sasa ni kibari
chakufanyia kazi nchini Ubelgiji.
Mzee samatta amesema mtoto wake huyo alitakiwa
kupewa kibari hicho mapema lakini walikuwa wanamuwekea vikwazo vingi hadi
kushihwa kupewa kibari hicho hadi sasa.


Amesema baada ya kushindikana kupatikana kibari
hicho kwa wakati muafaka ndipo serikali ya nchini Tanzania ikaingilia kati na
kuamuru Mbwana Samatta kupewa kibari hicho kabla ya kufikia siku ya kesho.
Mbwana Samatta kabla ya kwenda nchini Ubelgiji
alikuwa mchezaji wa TP Mazembe ya nchini Congo kabla ya mmiriki wa klabu hiyo Moses
Katumbi hajamruhusu kuondoka kutokana na kumalizika kwa mkataba wake.
Post a Comment