Halloween Costume ideas 2015

TANGAZA NASI.

TANGAZA NASI.

MEXIME ASEMA SIMBA HAIMTISHI.




Klabu ya soka ya Mtibwa Sugar ya Manungu turiani Mkoani Morogoro imejinasibu kufanya vizuri na kutuma salamu kwa klabu ya soka ya Simba katika mchezo wao wa kesho utakaopigwa katika dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaaam.


Kocha mkuu wa klabu hiyo Mecky Mexime amesema amejipanga vyema katika mchezo wao wa kesho dhidi ya wapinzani wao hao huku akijisifu kuwasoma vizuri Simba walipokutana katika Kombe la mapinduzi Visiwani Zanzibar.

Mchezo wa kesho unatarajiwa kuwa mgumu kutokana na klabu zote mbili zinakutana kwa mara ya pili katika Ligi kuu soka Tanzania bara baada ya kukutana katika kombe la mapinduzi huku klabu ya Simba ikitolewa na Mtibwa katika hatua ya nusu fainali.

Mtibwa yenyewe ilitolewa katika hatua ya fainali baada ya kufungwa mabao 3-1 na watoza ushuru wa URA ya Uganda.

Mexime amesema pamoja na kutolewa na timu ya URA ya kutoka nchini Uganda lakini kwa sasa hawageuki nyuma kuangalia makosa yaliyofanyika ila wanachoangalia kwa sasa ni mchezo wao wa kesho ambao umeteka hisia kuwa ya mashabikia wa soka nchini.

Post a Comment

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget