
Klabu ya Manchester United
imekanusha kuwa wamekutana na meneja wa Bayern Munich Pep Guardiola kuhusu
uwezekano wa yeye kuchukua nafasi ya Louis van Gaal.
Guardiola mwenye umri wa miaka 45
anatarajiwa kuondoka Bayern majira ya kiangazi na amesema tayari ameshapata ofa
kadhaa kutoka katika klabu za Uingereza.
Klabu ya Manchester City ndio
wanaopewa nafasi kubwa ya kumnyakuwa kocha huyo lakini Chelsea na United pia
zimekuwa zikihusishwa na tetesi za kumtaka.
Bayern walikuwa wameweka kambi yao
ya mazoezi huko Doha, Qatar wakati Bundesliga ikiwa katika mapumziko ya majira
ya baridi na ligi hiyo inatarajiwa kuendelea tena leo ambapo timu hiyo
itakwaana na Hamburg.
Post a Comment