
Kocha mkuu wa klabu ya soka ya Manchester United Louis
van Gaal amethibitisha kuwa klabu yake kwa sasa inahitaji kumsajili beki katika
kipindi hiki cha usajili wa January.
Mashetani hao wekundu wamepata msukosuko katika
msimu huu baada ya kuumia kwa wachezaji wake muhimu katika safu ya ulinzi ambao
Antonio Valencia, Luke Shaw, Marcos Rojo, and Ashley Young.
"kama ukiangalia katika safu yetu ya ulinizi
unaweza ukawaona wachezaji Valencia, Shaw, Rojo, Darmian, Young - Darmian hao
ni kutokana na kuwa hapo fit na hivyo nahitaji kupata beki katika kipindi hiki",
Alisema Van Gaal.
Akihojiwa katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika
leo Van Gaal amesema kutokana na kupata majeruhi katika kikosi chake hivyo
lazima aingie sokoni kwaajili ya kupata beki ambae ataweza kuwatoa hapo walipo.
Lakini alipohojiwa kuhusu kibarua chake klabuni hapo
Van Gaaal alisema anamahusiano mazuri sana na wachezaji wake hilo ndio jambo
muhimu kwake na haoni sababu ya kuondoka katika klabu hiyo.
Post a Comment