
Uongozi wa klabu ya soka ya Simba umeendelea na
msimamo wake juu ya malipo yao ya Fedha wanazodai kutoka kwa klabu ya Etoile Du Sahel ya Tunisia
juu ya mauzo ya aliyekuwa mchezaji wao Emmanuel Okwi.
Haji Manara ambaye ni afisa habari wa klabu ya soka ya
Simba amesema pamoja na klabu hiyo kupeleka maombi yao Shirikisho la soka
Duniani FIFA juu ya kuilipa klabu ya Simba malipo hayo kwa awamu lakini wao
kama uongozi wamegoma kulipwa hivyo kutokana na deni hilo kuwa la muda mrefu
ambalo mpaka sasa wazidi kuzungushwa.
Simba inaidai Etoile Du Sahel sh milioni 300 kwaajili ya mchezaji huyo ambaye alikuwa anakipiga klabu hapo kabla ya kutimkia nchini Dermak.
Post a Comment