Katibu Mkuu wa Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF
Mwesigwe Selestine leo amefungua rasmi kozi ya makocha ya FIFA katika viunga
vya Hostel za Karume jijini Dar es Salaam kwa ngazi ya juu kwa upande wa
makocha wanawake.
Akifungua kozi hiyo Mwesigwe amesema ni jamabo ambalo
walikuwa wanalipigania kwa muda mrefu kuhakikisha nao wanawake wanapata mafunzo kama hiyo ya ukocha kutokana na wao kutopata fursa hiyo kwa muda mrefu sasa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Soka la wananwake nchini
TWFA Amina karuma amesema anawashukuru TFF kwa kuandaa kozi hiyo kwa upande wa
wanawake na ni moha la kuendelea soka la wanawake nchini.
Naye mkufunzi wa kozi hiyo Sunday Kayuni amesema kozi
hiyo ambayo ilianza jana ni ishara kubwa sana kwa soka la wanawake na kuwataka
makocha hao kutumia nafasi waliyopata kikamilifu ili kuwaendeleza soka la vijana na
wanawake kwa ujumla.
Post a Comment