
Klabu ya soka ya Simba imekanusha kufanya mazungumzo
na kocha Kim Poulsen raia wa nchini Denmark kama ambavyo taarifa za awali
zilizoripotiwa kuwa klabu hiyo imefanya mazungumzo na kocha huyo ili kuchukua
mikoba ya aliyekuwa kocha wao wa zamani Dlyan Kerr raia wa nchini Uingereza
baada ya kutimuliwa.
Afisa habari wa Simba Hajji Manara amesema wao kama
klabu bado hawajafanya mzungumzo na kocha huyo kama inavyoripotiwa katika
vyombo vya habari huku akikiri kufanya mazungumzo na kocha msaidizi wa timu ya
Taifa ya Tanzania Taifa Stars Hemed Morocco ambaye walishindwana kutokana na maslai
aliyokuwa anataka kocha huyo.
Hata hivyo Manara amesema kwa sasa wanampango wa kuangalia kocha nje ya Tanzania hasa katika bara la Afrika au nje ya bara la Afrika na jitihada hizo zinaendelea kwa haraka zaidi ili kumpata kocha mpya wa klabu hiyo.
Post a Comment