Gerard Pique ametajwa kuwa
mwanamichezo bora wa Catalan katika sherehe za 19 za Michezo za Catalan
akiwatimulia vumbi Andres Iniesta na Messi
Mlinzi wa kati wa Barcelona Gerrard
Pique ametangazwa mchezaji bora wa Catalan wa mwaka 2015.
Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United amewapiku wapinzani wenzake akiwemo kiungo wa Barcelona Andreas Iniesta.
Beki huyo wa Barcelona mwenye umri wa miaka 28 alikuwa na mchango mkubwa kwa timu yake kutwaa mataji matano 2015 ikiwa ni pamoja na lile la Ligi ya Mabingwa.

"Katika taaluma kuna nyakati mbaya na nzuri Katika nyakati nzuri hupaswi kufikiri kwamba wewe unafanya vizuri kuliko yeyote mwingine na katika nyakati mbaya usifikiri kuwa unafanya vibaya kuliko wote",alisema Pique.
Hali kadhalika Barcelona imetajwa kuwa timu bora ya Catalan katika hafla hiyo
iliyofanyika katika makumbusho ya jiji hilo.
Pique alianza taaluma yake ya
soka Nou Camp katika akademi maarufu kama La Masia, lakini kabla ya kuingia
kwenye timu ya wakubwa alijiunga na Manchester United 2004.
Hata hivyo alipitia kipindi kigumu kwa kukosa namba kikosi cha kwanza akiwa Uingereza na Real Zaragoza alipocheza kwa mkopo, aliuzwa Barca miaka minne baadaye, mahali ambapo ameendelea na kuwa beki bora wa kati duniani.

Post a Comment