
Siku moja baada ya Azam kusafiri kwenda nchini Zambia kucheza mashindano maalum ya mualiko, hatimaye Simba na Yanga nazo zimeamua kufanya ziara zake za mazoezi.
Ligi kuu Tanzania Bara imepumzika kwa muda baada ya
mechi za duru la kwanza kumalizika wiki iliyopita huku la pili likitarajiwa
kuendelea mwishoni mwa wiki hii.
Wakati Ligi hiyo ikiwa kwenye mapumziko mafupi,
michuano ya kombe la FA imekuwa ikiendelea kuchezwa.
Lakini Yanga imeibuka na kudai kwamba ipo mbioni
kusafiri kwenda nchini Afrika Kusini kucheza mechi kadhaa za kirafiki ili
kujiweka fiti zaidi.
Mkuu wa Kitengo cha habari cha Yanga, Jerry Muro
amesikika akisema kwamba wataondoka nchini Ijumaa kwa ajili ya kambi hiyo.
Kambi ya Yanga inatarajia kuwa katika mji wa Johannesburg
ambako itaweka kambi inayotarajiwa kuwa ya zaidi ya siku tano.
Kama hiyo haitoshi, kutoka kwa Simba SC kuna taarifa
za uhakika zinaeleza kwamba nao wako mbioni kusafiri juma hili kwenda Kenya kwa
ajili ya kushiriki mashindano maalum.
kwa sasa wanasubiriwa simba kuona je kweli na wao wataondoka nchini kuelekea nchini kenya
Post a Comment