
Klabu ya soka ya Simba imeendelea kushikilia msimamo
wake huku ikiipa masharti Shirikisho la soka nchini TFF kuhakikisha ratiba ya
Ligi kuu soka Tanzania bara haibadirishwi na kubaki vile vile kama ilivyo
pangwa kwa michezo ya mwishoni mwa wiki hii kuendelea.
Afisa habari wa klabu ya soka ya Simba Haji Manara
amesema wataendelea kushikilia msimamo huo huku akiitaka TFF kuhakikisha kila
klabu inacheza michezo yake yote bila kuwa na timu yoyote inayoweka viporo vya
kucheza.
Hatua hiyo imekuja baada ya klabu ya soka ya Azam Fc
kupewa ruhusa na TFF kueleke nchini Zambia kwaajili ya kucheza michezo ya kirafiki
ya kujiweka sawa na mashindano ya kombe la Shirikisho kwa bara la Afrika hivyo
kupelekea michezo yao ya ligi kuu kusogezwa mbele.
Post a Comment