
Mshambuliaji Amis Tambwe amedizi kuonyesha thamani
yake leo hii na kuifanya klabu yake ya zamani ya Simba ijutie kumtoa mchezaji
huyo kwa watani zao hao wa jadi katika kipindi kilichopita na kuwafanya wazidi
kuadhirika kwa kutoona umuhimu wake.
Tambe alikuwa shujaha hii leo baada ya kuwapatia
mabingwa ligi kuu soka Tanzania bara ushindi wa mabao matatu kati ya 5-0 walioshinda
siku ya leo dhidi ya klabu ya Maji maji Fc.
Wakati Tambwe raia wa Burundi akifanya
mauaji hayo yakufunga mabao matatu Wazimbabwe, Donald Ngoma na Thabani Kamusoko
na wao wamonesha kuwa hawajaja nchini kushanga mataa na kufunga bao moja moja
kila mmoja.
Post a Comment