
Kiungo wa zamani za Bolton Wanderers, Newcastle
United na West Ham United, Kevin Nolan anatarajiwa kutangazwa kama
kocha-mchezaji wa klabu ya Leyton Orient ya Ufaransa kwa mkataba wa miaka
miwili na nusu.
Mshambuliaji nyota wa kimataifa wa Brazil, Neymar na
baba yake wameripotiwa kukutana na wawakilishi wa Real Madrid katika sherehe za
utoaji tuzo za Ballon d’Or kujadili uhamisho baada ya mazungumzo ya mkataba
mpya na Barcelona kusimama.
Fulham itakuwa tayari kumuuza mshambuliaji wake
Moussa Dembele kwa paundi milioni sita kwenda Tottenham Hoptspurs kipindi hiki
cha Januari lakini watamuhitaji tena kwa mkopo mpaka mwishoni mwa msimu.
Imeiripotiwa kuwa Chelsea wanakaribia kumsajili
nyota wa kimataifa wa Brazil Alexandre Pato, hatua hiyo inaweza kushindikana
baada ya Sporting Lisbon nao kutajwa kumuwania mchezaji huyo huku tayari wakiwa
wameanza mazungumzo.
Post a Comment