
Baada ya klabu ya soka ya Tanzania Prison kushinda
hii kwa mabao 2-1 dhidi ya Coastal Union katika mchezo uliochezwa uwanja wa
Sokoine jijini Mbeya mashabiki wa timu hiyo wameiponda klabu ya Mbeya City
ambao ni majirani zao kwa kutandikwa mabao 2-1dhidi ya Ndanda.
City hii leo wakipigwa kipigo kizito cha mabao 4-1
na Ndanda Fc, mechi hiyo imechezwa katika dimba la uwanja wa Nangwanda Sijaona
mkoani Mtwara.
Azam yenye imerudi kileleni kwa kufikisha pointi 39
na kuishusha Yanga ambayo ina pointi 36 na ambayo kesho Alhamisi inashika
dimbani dhi ya maji maji.
Azam wamepanda kileleni baada ya kuifunga Mgambo JKT
bao 2-1, mechi iliyochezwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Mabao ya Prisons yalifungwa na Jeremiah Juma dakika
ya 61 baada ya kupiga shuti kali na kutinga nyavuni ikiwa ni piga nikupige
langoni mwa wapinzani wao wakati bao la pili lilifungwa na Mohamed Mkopi dakika
ya 82.
Mkopi alifunga bao hilo baada ya kupokea krosi ya
Benjamini Asukile huku bao la kufutia machozi la Coastal Union likifungwa na
Mtenje Juma dakika ya 76 akiunganisha krosi ya Amad Juma.
Post a Comment