
Klabu ya soka ya Young Africans siku
ya kesho watawakaribisha timu ya Friends Rangers katika dimba la uwanja wa
Taifajijini Dar es Salaam.
Yanga inashuka dimbani kesho ukiwa
ni Mchezo huo ni wa kombe la shirikisho baaada ya kusimam kwa ligi kuu soka Tanzania
bara.
Michezo mingine ya kombe hilo ni Njombe
Mji watakua wenyeji wa Tanzania Prisons katika uwanja wa Amani Njombe, huku
Stand United wakicheza dhidi ya Mwadui FC katika uwanja wa Kambarage mjini
Shinyanga.
Michuano hiyo itaendelea Jumatatu,
Kagera Sugar wakiwa wenyeji wa Rhino Rangers katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi
mjini Tabora, Panone FC dhidi ya Madini FC uwanja wa Ushirika mjini Moshi na
Africa Lyon wakiwa wenyeji wa Azam FC uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.
Jumanne Mtibwa Sugar watawakaribisha
Abajalo FC uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, Lipuli dhidi ya JKT Ruvu uwanja wa
Wambi Mafinga, Africa Sports dhidi ya Coastal Union Mkwakwani jijini Tanga, na
Geita Gold watakua wenyeji wa Mgambo Shooting katika uwanja wa Nyankumbu mjini
Geita.
Singida United watacheza dhidi ya
Mvuvuma siku ya Jumatano katika uwanja wa Namfua mjini Singida, na mchezo wa
mwisho utachezwa Februari Mosi katika ya Wenda FC dhidi ya Mbeya City uwanja wa
Sokoine jijini Mbeya.
Post a Comment