
Kuelekea katika kipute cha kesho kinachozikutanisha
klabu hasimu zaidi nchini Uingereza klabu ya Arsenal dhidi ya Chelsea mchezaji
wa zamani wa klabu ya soka ya Arsenal Patrick Vieira amemponda bosi wake wa zamani
Arsene Wengwer.
Viera amesema aliyekuwa kocha wa zamani wa klabu ya
soka ya Chelsea Jose Mourinho ni bora
zaidi kuliko kocha wake wa zamani babu Arsene Wenger.
Mchezaji huyo ambaye ameitumikia The Gunners kwa miaka
9 ameshinda makombe matatu ya Ligi na makombe manne ya FA Cup kabla ya kutimkia
katika klabu ya Juventus na baadae Inter ambapo alifanya kazi kwa muda na Mourinho.
Viera ambaye ni raia wa nchini Ufaransa amesema
amefanya kazi na Mourinho kwa muda lakini ameona ni bora zaidi kuliko kocha wake
huyo wa zamani wa Arsenal.
Akihojiwa Viera amesema Mourinho ndiye aliyemfanya
apende kazi yake ya ukocha na alikuwa alikuwa anajua mazuri na mabaya ya soka.
Post a Comment