
Klabu ya soka cha Uchina ,Guangzhou Evergrande,
kimevunja rekodi ya nchi hiyo kwa kima cha fidia ya kumsajili mchezaji katika
timu yao.
Klabu hiyo imelipa dolla million 45 kusajili huduma
za mshambuliaji wa kutoka Colombia,Jackson Martinez.
Martinez ambae sasa ameihama timu ya uhispania
Atletico Madrid ametia sahihi kandarasi ya miaka minne.
Aliwahi kuifungia Atletico mabao 22 baada ya kuhamia
Uhispania kutoka Porto na yeye ndiye mchezaji wa kiwango chake kuhamia Uchina
baada ya kiungo cha kati wa Chelsea Ramires kuhamia Jiangsu Suning.
Kwa kutumia kitita kikubwa namna hiyo sasa ligi kuu
ya Uchina inaikurubia ligi ya Uingereza kwa kima cha fedha zinazotumuka katika
kuendesha soka nchini humo.
Post a Comment