
RAIS wa klabu ya soka ya Atletico Madrid Enrique
Cerezo amethibitisa kuwa klabu yake inataka kumsajili tena mshambuliaji wa
klabu ya soka ya Chelsea Diego Costa.
Costa alijiunga na mabingwa hao watetezi wa Stamford
Bridge kwa ada ya uhamisho £32 million July 2014 na ameisaidia klabu yake hiyo
kutwaa ubingwa wa ligi kuu nchini Uingereza msimu uliopita.
Mchezaji huyo mwenye miaka 27alihusishwa kurudi Atletico,
ambako alishinda kombe la La Liga kuifikisha klabu yake katika michuano ya Ligi
ya mabingwa barani Ulaya katika kipindi hiki kama akiachiwa.
Post a Comment