
Kuelekea katika mchezo wa ligi ya mabingwa usiku huu kati ya Chelsea na PSG kiungo wa klabu ya Chelsea Eden Hazard amekiri kuwa klabu yake wanaiogopa Paris Saint-Germain katika mechi yao ya Ligi ya Mabingwa Ulaya katika raundi ya 16-mtoano.
Kiungo huyo amebainisha kuwa The Blues hawakufurahi
kusikia kuwa wamepangwa kucheza dhidi ya timu hiyo ya Ligue 1 Ligi ya Mabingwa
kwa mara ya tatu mfululizo.
Hazard amesema hajasahau klabu yao ilitolewa na PSG katika
hatua hii msimu uliopita baada ya timu
hiyo ya Uingereza kuibuka mshindi walipokutana robo fainali mnamo 2012-14.
Hazard amemtaja Marco Verratti kama mchezaji hatari
wa PSG katika mechi yao ya leo na amesema ni habari njema kwa Chelsea kwamba
Muitaliano huyo bado anaendelea kupona majeraha na hatacheza mechi hiyo, lakini
amewataja Zlatan Ibrahimovic na Angel Di Maria kuwa hatari nyingine kwao.
Post a Comment