
Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo
ameondoka kwa hasira katika katika chumba cha mahojiano baada ya kuulizwa juu
ya rekodi ya ufungaji magoli katika mechi za ugenini msimu huu.
Ronaldo mwenye miaka 31, amefunga magoli 32 msimu
huu lakini hajafunga akiwa ugenini tangu mwezi Novemba mwaka jana.
Ronaldo alikuwa akiongea na wanahabari kabla ya
mechi ya leo Jumatano ya Real Madrid dhidi ya Roma katika dimba la Stadio
Olimpico.
Mwezi Disemba mwaka jana, mreno huyo alikuwa
mchezaji wa kwanza kufunga magoli 10 katika mchuano wa makundi.
Goli lake la 11 ni la ugenini lakini hajafunga
katika mechi nne za ugenini.
Post a Comment