
Klabu ya PSG kutoka Ufaransa imepata ushindi wa
mabao 2-1 dhidi ya Chelsea katika mechi ya mkondo wa kwanza ya Ligi ya Klabu
Bingwa Ulaya huku Benfica nao wakiilaza Zenit St-Petersburg.
Paris St-Germain walipata bao la kuongoza kupitia kwa
mshambuliaji matata wa Sweden Zlatan Ibrahimovic kunako dakika ya 39.
Chelsea walisawazisha katika dakika ya 45 kupitia
kwa Mikel Obi lakini Edison Cavan akaitumia dakika ya 78 kuwaumiza Chelsea.
Bao hilo la Mikel ndilo lake la sita kufungia
Chelsea katika karibu miaka 10 aliyokaa katika klabu hiyo ya Uingereza.
Bao pekee la Benfica, waliokuwa nyumbani, lilifungwa
na Jonas muda wa ziada kutokana na mkwaju wa adhabu uliopigwa na Nicolas
Gaitan.
Hilo ndilo bao lake la 25 msimu huu na la 45
kufungia Benfica katika mechi 56 tangu alipojiunga nao akitokea Valencia mwaka
2014.
Zenit walisalia wachezaji kumi uwanjani baada ya
Domenico Criscito kupewa kadi ya pili ya njano dakika ya 90.
Mechi zingine mbili zitapigwa usiku wa leo ambapo…
KAA Gent
vs VfL Wolfsburg
Roma vs Real Madrid
Post a Comment