
Mamia ya watu wakiwemo wasanii wa muziki wa kizazi
kipya leo wamejitokeza kwenye hospitali ya Muhimbili kumuaga marehemu Michael
Mhina maarufa kama John Walker aliyefariki dunia Jumanne jijini Dar es salaam.
Walker ameagwa mchana wa leo na kisha mwili wake
kusafirishwa kwenda jijini Tanga kwa ajili ya maziko.
Msanii huyo alifariki dunia baada ya kulipukiwa na
mtungi wa gesi wakati akiutengeneza.
Inaelezwa kuwa mtungi huo wa gari ulilipuka na
baadhi ya vipande vya chuma vikamjeruhi kichwani na kumfanya akimbizwe
hospitali ya Muhimbili na huko ndiko mauti yalipomkuta.

Msanii huyo kutoka katika kundi la muziki la Watukutu
alikuwa maarufu kutokana na kuimba mistari yenye ujumbe lakini kwa sauti ya
mlevi.
Ndugu, jamaa na marafiki wakiwemo wasanii wa muziki
wa kizazi kipya wamepta fursa ya kumuelezea marehemu John Walker.
Post a Comment