Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim
Majaliwa leo amefanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujezi wa uwanja wa Uhuru
maarufu shamba la bibi na kupitia maeneo mbalimbali ya Uwanja wa taifa jijini Dar
es Salaam.
Katika ziara hiyo, Majaliwa aliambatana na Waziri wa
Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye pamoja na katibu wa wizara
hiyo Elisante Ole Gabriel.
Pamoja na ukaguzi huo Waziri mkuu Majaliwa alionyeshwa
ramani ya uwanja wa Uhuru inayoonesha uhalisia pindi ukarabati wake utakapokamilika.
Mbali na ukaguzi huo Majaliwa alikutana na kuteta na
vyama mbalimbali vya michezo kwa lengo la kupokea changamoto zinazowakabili na
kujadili maendeleo ya michezo nchini.
Kitaaluma Waziri mkuu, Majaliwa ni kocha wa mpira wa
miguu ambapo kwa sasa ana cheti cha kozi ya leseni B ya ukocha, inayompa nafasi
ya kufundisha klabu yoyote ya Ligi Kuu hapa nchini.
Post a Comment