Kampuni ya Tigo kwa kusaidiana na Azam Media leo
wamefanya uzinduzi wa Promosheni ya kujishindia safari ya kwenda kushuhudia mechi
ya Ligi Kuu ya Hispania maarufu kama La Liga, kati ya klabu ya soka ya Deportivo
la Coruna na Barcelona Machi mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Idara ya
Masoko ya Azam TV, Mgope Kiwanga amesema ni nafasi nzuri kwa wapenda soka
kushiriki katika promosheni hiyo ili kuweza kutimiza ndoto zao za kwenda nje.
Naye Meneja Promosheni hiyo kutoka wa Tigo Pesa,
Mary Rutta amesema wameona wateja wao wengi ni wafatiliaji wa mchezo wa mpira
na hiyo wameamua kuwaongezea burudani zaidi katika promosheni hiyo.
Ili kushiriki, unatakiwa kulipia kifurushi cha Azam
Sports HD kwa miezi miwili kwa bei ya punguzo, Sh 22,000 kupitia Tigo Pesa na
utaingia kwenye droo, ambayo washindi wengine 10 watapata zawadi mbalimbali
kila wiki zikiwemo jezi za kiwango cha juu cha ubora, fulana za La Liga, mpira
wa ubora wa hali ya juu, peni, cha kushikia funguo, miwani ya La Liga Na
nyinginezo.
Post a Comment