
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limewaonya
viongozi wa vilabu, wachezaji, waamuzi na wasimamizi wa mchezo kutojihusisha na
upangaji wa matokeo (Match fixing) katika michezo inayoendelea sasa katika ligi
za ngazi mbalimbali za nchini.
TFF imejipanga na inasimamia vizuri michezo ya Ligi
Kuu (VPL), Daraja la Kwanza (FDL), Daraja la Pili (SDL) na Azam Sports
Federation Cup (ASFC) inayoendelea na yoyote atakayebainika kujihusisha na
mchezo huo wa upangaji matokeo, hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa.
Katika michezo yote inayoendelea TFF ina maofisa
wake wanaofuatilia kwa ukaribu michezo hiyo, hivyo endapo kiongozi, mchezaji,
msimamizi au mwamuzi atabainika kujihusisha na upangaji wa matokeo hatua kali
zitachukuliwa .
TFF inawaomba viongozi, wachezaji, wasimamizi wa
michezo na waamuzi kutojihusisha na mchezo huo wa upangaji wa matokeo kwani
kufanya hivyo ni kukiuka katiba, sheria na kanuni zinaongoza mpira wa miguu
nchini.
Post a Comment