
Klabu ya Leicester City wamezidi kuonyesha makali yao
na kuongeza harakati za kuwa mabingwa msimu huu baaada ya kuitandika klabu ya Crystal
Palace bao 1-0 na kujiweka katika mazingira mazuri ya msimamo wa ligi kuu soka
nchini Uingereza.
Msimu huu unaweza ukawa watofauti kidogo kwa mashabiki
wa klabu kubwa nchini Uingereza na inawezekana kocha Claudio Ranieri akazidi
kuwatia joto makocha waliozoeleka katika ligi hiyi baada ya klabu yake
kuonyesha cheche zaidi msimu huu.

Jamie Vardy na Riyad Mahrez unaweza ukawa ndio msimu
wao wa mwisho kuendelea kukipiga nchini Uingereza kutokana na klabu nyingi
kuonyesha nia ya kuwahitaji wachezaji hawa.
Post a Comment