Klabu ya soka ya Simba imeendeleza rekodi yake na wimbi
la ushindi Jumamosi ya leo kwa kuifunga Coastal Union mabao 2-0 katika uwanja
wa Mkwakwani Mkoani Tanga.
Shukrani kwa Danny Lyanga na Hamis Kiiza kwa kupachika
bao moja moja kwa kila mmoja na kuifanya Simba kupata pointi tatu ka kujikunjia
kibindoni jumla ya pointi 57 baada ya kucheza michezo 24 ya ligi kuu ya Tanzania
bara.
Simba sasa inaongoza ligi kwa tofauti ya pointi saba
dhidi ya wapinzani wake Yanga na Azam zenye pointi 50 kila moja huku zikiwa
zimecheza mechi 21 mechi tatu nyuma ya Simba.
Post a Comment