
Kikosi cha Yanga jumamosi hii kinatarajiwa kushuka
dimbani katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuvaana na
timu ya APR ya kutoka nchini Rwanda.
Yanga inashuka dimbani kucheza na APR katika dimba
la uwanja wa Taifa ka ajili ya kutafuta tiketi ya kushiriki Fainali za kombe la
klabu bingwa Afrika.
Katika mchezo wao wa kwanza uliopigwa katika dimba
la Amahoro Kigali nchini Rwanda Yanga ilipata ushindi wa mabao 2-1 na kuifanya kuongeza
matumaini ya kupata ushindi zaidi jumamosi hii na kuifanya isonge mbele.
Wakati Yanga wakijitupa jumamosii hii dimbani, siku Jumapili
Azam FC watakua wakicheza dhidi ya Bidvest FC kutoka nchini Afrika Kusini
katika mchezo wa Kombe la Shirikisho (CAF CC) kwenye uwanja wa Azam Complex
Chamazi.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
limezitakia kila la kheri vilabu wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya
kimataifa, timu za Azam FC na Yanga SC katika michezo yao watakayocheza
wikiendi hii.
Katika salamu hizo, TFF imezitakia kila la kheri
timu hizo kuhakikisha zinafanya vizuri katika michezo yao ili ziweze kusonga
mbele katika hatua inayofuata, na kuwapa furaha washabiki wa mpira wa miguu
pamoja na watanzania wote.
Post a Comment