
picha kwa msaada wa TFF.
Timu ya soka ya wanawake Twiga Stars imeeondoka
ijumaa hii kuelekea nchini Zimbabwe kuwafata wazimbabwe katika mchezo wa
marudiano wa kusaka tiketi ya kushiriki fainali za Afrika kwa upande wa
wanawake.
Kocha mkuu wa Timu ya Twiga Stars Nasra Juma amesema
kuelekea katika mchezo wao huu kikosi chake kimejiaandaa vyema na wanaimanai
watashinda na kusonga mbele akatika hatua inayofata ya kushiriki michuano hiyo
kwa upande wa wanawake.
Tigwa Stars inasafiri kuelekea nchini Zimbabwe kucheza
mchezo wake huo huku ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wake kwanza katika
dimba la uwanja wa Azam Complex uliopo chamazi jijini Dar es Salaam.
Mchezo huo wa Twiga Stars na timu ya Zimbabwe
unatarajiwa kupigwa march 20 mwaka huu nchini Zimbabwe.
Mkuu wa msafara ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji na
Mwenyekiti wa Kamati ya Soka la Wanawake TFF, Amina Karuma, benchi la ufundi
litaongozwa na kocha mkuu Nasra Juma, kocha msaidizie Elyutery Muholery, kocha
msaidizi Edina Lema, daktari wa timu Anange Lwila, mtunza vifaa Esther
Chaburuma na meneja wa timu Furaha Francis.
Wakati timu ya Twiga ikisafiri ijumaa hii nao kaka
zao Taifa Stars inatarajiwa kuondoka siku ya jumamosi kuelekea nchini Chad
kwaajili ya kuwafata wa Chad katika mchezo wao wa kuwania kufuzu fainali za
Afrika kwa upande wa wanaume.
Post a Comment