
IKIWA inaendelea na mazoezi ya kujiandaa na mchezo
wa ligi kuu dhidi ya Mbao Fc uliopangwa
kuchezwa mwishoni mwa juma hili kwenye uwanja wa CCM Kirumba, Mbeya City
fc inataraji kuondoka mjini
Shinyanga ijumaa hii kuelekea jijini
Mwanza tayari kwa kuikabili timu hiyo iliyopanda daraja kwa ‘mtereko’ tiketi ya mezani.
AFISA HABARI wa kikosi hiki, Dismas Ten, amesema kuwa
City itaondoka mjini Shinyanga ijumaa
jioni kuelekea jijini Mwanza ikiwa na lengo moja tu la kuvuna pointi tatu zingine kwenye uwanja wa CCM Kirumba kama
ilivyokuwa kwenye mchezo wa juma lililopita dhidi ya wenyeji Toto
Africans.
Ten aliweka wazi kuwa kiungo Geoffrey Mlawa na mshambuliaji Omary Ramadhani waliyopata
majeraha kwenye mchezo uliopita dhidi ya Toto Africans wamerejea kwenye
hali nzuri na anaweza kuwa sehemu ya mchezo huo wa jumamosi endapo
Mwalimu Kinnah Phiri atapenda kuwatumia.
Post a Comment