Kocha Kinnah Phiri ameanza kukinoa
kikosi chake kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara
dhidi ya Azam Fc uliopangwa kuchezwa
kwenye uwanja wa Sokoine jijini hapa
siku ya jumamosi.
Afisa habari wa klabu ya Mbeya City Dismas
Ten amesema kuwa nyota wote 30 ikiwa ni pamoja na 25 waliokuwa
nje ya jiji la Mbeya kwa takribani wiki tatu kwa ajili ya michezo ya mwanzo wa
msimu wamejumuika kwenye mazoezi ya leo kwenye uwanja wa Sokoine.
Ten amesema kuwa huu ni msimu ambao
City imejipanga kuvunja rekodi zote ambazo ilikuwa haijawahi
kuzifikia tangu ilipopanda daraja misimu
mitatu iliyopita.
Post a Comment