Kikosi cha timu ya cha Kilimanjaro Queens kesho kinashuka dimbani kukipiga dhidi ya timu ya wanawake kutoka nchini Burundi ukiwa ni mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya Challenge.
Mwenyekiti
wa soka la wanawake nchini Amina Karuma amesema kwa upande wa hali za wachezaji
ni nzuri na wapo tayar kwa mchezo wao huo wa kujipima uwezo.
Kikosi hicho cha Kilimanjarao Queens
baada ya mchezo huu a kujipima uwezo kinatazamiwa kuelekea mjini Jinja kuanza
rasmi michuano ya kuwania kucheza fainali za kombe la Mataifa ya Afrika
Mashariki na kati Challenge.
Kwa Upande mwingine Karuma amesema
wanaendelea na maandalizi ya ligi ya wanawake amabyo inatarajiwa kuanaza
kutimua vumbi lake mwezi Oktoba mwaka huu.
Post a Comment