BAADA ya safari ndefu ya saa kadhaa, kikosi cha
Mbeya City Fc tayari kimewasili jijini Mbeya kujiwinda na mchezo ujao wa ligi
kuu soka Tanzania bara dhidi ya Azam Fc
uliopangwa kuchezwa mwishoni mwa juma hili kwenye uwanja wa Sokoine.
Kocha wa timu hiyo Kinnah Phiri ameamua kuwapa
mapumziko ya siku moja wachezaji wake ili waweze kupumzika kutokana na uchovu
wa safari ndefu na leo wameingia kwenye uwanja wa Sokoine kuanza mazoezi ya matayarisho ya mchezo huo
wa jumamosi.
Kwenye michezo mitatu iliyopita City
ilifanikuwa kuibuka na pointi 7,
kufuatia suluhu ya bila kufungana na Kagera Sugar na baadae kuiadhibu Toto
Africans bao 1-0 na mwisho kuhitimisha kwa kuifunga Mbao Fc bao 4-1 na kushika usukuni wa ligi kuu ya soka Tanzania bara.
Post a Comment