Michuanao ya Airtel Rising Stars imefunguliwa Rasmi
Jumanne hii kwa ngazi ya Taifa huku ikishuhudiwa timu za wasichana kwa wanaume wenye
umri chini ya miaka 17 zikishuka dimbani kupambana.
Afisa Mahusianao wa kampuni ya Airtel Jane Matinde
amesema kwa upande wao wanajuvunia sana kuendeleza vipaji hivyo vya watoto na
kuvifanya kuonekana kwa makocha mbalimbali hapa nchini na kuwafanya vijana hao
kutimiza ndoto zao za kucheza soka.
Kwa upande wake kocha wa timu ya wasichana kutoka Lindi
Shaibu Issa amesema kwa upande wao ni mara ya kwanza kushiriki katika michuano
hiyo na kupoteza mchezo wao dhidi ya timu ya Arusha kumewapa somo zaidi la
kujua mbinu mbalimbali za michuano hiyo.
Nao wachezaji wa timu hiyo ya lindi ambao leo hii
walipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya timu ya Arusha wamesema ugeni wao ndi chazo cha wao kupoteza mchezo huo.
Post a Comment