Baada ya kuwasili nchini kwa Timu ya Taifa ya
Tanzania Taifa Stars, Kocha Mkuu wa timu hiyo Charles Boniface Mkwasa amefunguka
na kuelezea kilichowasibu wao kupoteza mchezo wao dhidi ya timu ya Taifa ya
Nigeria katika mchezo wa kumaliza kukamilisha
ratiba ya kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa Afrika.
Mkwasa amesema kutojipanga vyema kwa Shirikisho la
soka nchini Tanzania TFF kumechangia kwa kiasi kikubwa timu hiyo kutofanya
vyema katika mchezo wake huo kutokana na kutawala kwa siasa nyingi za kukosa
fedha kwa TFF hali inayosababisha timu hiyo kutoweza kuwa na programa ya
mazoezi kwa wakati unaotakiwa.

Mkwasa hakuishia hapo pia alielezea misukosuko ya
safari yao na hii inasababishwa na kutokuwa makini kwa TFF na kutojiandaa vyema
kumesababisha hata katika safari yao kuwepo kwa mizengwe mingi kutokana na
wasafirishaji wao kushindwa kuwapa huduma nzuri kwa wakati unaotakiwa.
Kwa upande mwingine Mkwasa amegoma kupewa kwa Adhabu
kwa beki kisiki Kelvin Yondani kwa kuonyesha utovu wa nidhamu wa kutosafiri na
timu na kuelezea kwa upande wake haoni kama inamaana ya kumpa adhabu bali ni
TFF kuhakikisha wanaongeza motisha kwa wachezaji wa timu ya Taifa.
Post a Comment