
Mshambuliaji wa klabu ya soka ya Barcelona Lionel
Messi anaweza akasaini mkataba mpya ndani ya klabu hiyo kwa msimu huu mpya wa
ligi.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo Robert
Fernandez amesema Messi's mkataba wake unamalizika msimu wa mwaka 2017-18 na
anaweza akaongeza mkataba mpya msimu huu.
Klabu ya Barcelona tayari imeshawaongezea mikataba
mipya wachezaji wake Neymar, Rafinha, Sergio Busquets na Javier Mascherano, na Fernandez
amesisistiza kuwa Messi naye atafuata
nyayo za wenzake.
Post a Comment