
KIUNGO mpya wa Chelsea, N’Golo Kante amefanunua
jinsi gani alivyokataa ofa ya meneja wa Manchester United Jose Mourinho kwa
ajili ya kujiunga na Chelsea kiangazi hiki.
Nyota huyo alijiunga na Chelsea akitokea Leicester
City kwa kitita cha paundi milioni 29, lakini ilikuwa baada ya kukataa kwenda
kuichezea United.
Akihojiwa Kante amesema lilikuwa ni jambo zuri
Mourinho kumpigia, ingawa alishaonywa toka awali jinsi gani atakavyomshawishi.
Kante aliendelea kudai kuwa alimsikiliza meneja huyo
lakini wakati huo tayari alishafanya maamuzi kwamba aidha abaki Leicester au
aende Chelsea.
Post a Comment