
KOCHA mpya wa timu ya taifa ya Ubelgiji, Roberto
Martinez ameanza vibaya kibarua chake hicho baada ya kuchapwa mabao 2-0 katika
mechi ya kwanza dhidi ya Hispania na kujikuta akizomea na mashabiki
waliojitokeza kushuhudia mchezo huo.
Martinez raia wa Hispania mwenye umri wa miaka 43,
aliteuliwa kushika nafasi hiyo Agosti 3 mwaka huu ikiwa imepita miezi mitatu
toka atimuliwe Everton.
Akihojiwa kuhusiana na hilo, Martinez amesema ni
jambo lisilowezekana kutegemea mabadiliko makubwa katika kipindi kifupi hivyo
mashabiki wanapaswa kuwa na subira.
Katika mechi zingine za kirafiki za kimataifa
zilizochezwa jana, Ufaransa ilifanikiwa kuichapa Italia mabao 3-1, Ugiriki
ikiichapa Uholanzi kwa mabao 2-1 wakati mabingwa wa Ulaya Ureno wakiiburuza
Gibraltar kwa mabao 5-0.
Post a Comment