
MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Argentina, Lionel
Messi amerejea kwa kishindo kulitumikia taifa lake baada ya kufunga bao pekee
katika ushindi wa bao 1-0 waliopata dhidi ya Uruguay katika mchezo wa kufuzu
michuano ya Kombe la Dunia.
Messi alitanagza kustaafu soka la kimataifa baada ya
Argentina kupoteza mchezo wa fainali wa michuano ya Copa America dhidi ya Chile
kiangazi hiki lakini alibadili uamuzi wake wiki kadhaa baadae.
Nyota huyo wa Barcelona alifunga bao hilo katika
dakika ya 43 ya mchezo huku Argentina wakimaliza wakiwa pungufu baada ya Paulo
Dybala kutolewa kwa kupewa kadi ya pili ya njano.
Katika michezo mingine iliyochezwa kwa upande wa
Amerika Kusini, Colombia iliitandika Venezuela kwa mabao 2-0, Bolivia ikiichapa
Peru kwa mabao 2-0 huku mabingwa wa bara hilo Chile nao wakichapwa na Paraguay
kwa mabao 2-1.
Post a Comment