
Mashabiki wa klabu ya soka ya Simba wameelezea
furaha yao juu ya uimara wa kikosi chao cha wekundu wa msimbazi kuwa bora zaidi kuliko timu nyingine kwa msimu
huu mpya wa ligi kuu soka Tanzania bara na kujihakikishia lazima kitatwaa
ubingwa wa ligi hiyo.
Mashabiki hao wamesema
kutokana na usajili uliofanya na uongozi wao kwa kuwaleta wachezaji waliona
uwezo wa kusakata kabumbu ni wazi kuwa ligi ya msimu huu kwa upande wao ni
mchekea tuu.
Klabu ya soka ya Simba jumamosi hii inashuka dimbani
kukipiga dhidi ya timu ya polisi Dodoma inayoshiriki ligi daraja la kwanza
ukiwa ni mchezo wa kirafiki lakini pia ni kuunga mkono kauli ya Rais Mhe.Dkt John
pombe Magufuli juu ya kuhamia mjini Dodoma kwa Wizara nyeti za Serikali.
Post a Comment