WITO umetolewa kwa watanzania wote kuhakikisha
wanaiunga mkono timu ya Taifa ya Tanzania ya vijana umri chini ya 17 katika
mchezo wake wa mwisho dhidi ya timu ya vijana ya nchini Congo mchezo
utakaopigwa Septemba 18 mwaka huu.
Haya yamesemwa na kocha Mkuu wa Timu hiyo Bakari
Shime kuelekea katika mchezo wao huo huku pia timu hiyo ikijiandaa na kuelekea
nchini Shelisheli kuweka kambai ya muda mrefu kwa ajili ya maandalizi ya mchezo
huo.
Shime amesema kwenda kuipokea timu hiyo ikirudi na
ubingwa haina maana sana zaidi ya kuisapoti timu hiyo katika mchezo huo hasa ukizingatia
ikifanikiwa kuitoa timu hiyo inakuwa imejiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu
hatua inayofuata.
Post a Comment