Klabu ya soka ya Atletico Madrid wameibana mbavu klabu ya soka ya Barcelona ikiwa kwake Camp Nou na kufanikiwa kupata sare ya bao 1-1 katika mechi yao ya tano ya La Liga.
Bao la Barcelona liliwekwa kimiani na mchezaji Ivan Rakitic katika dakika ya 41ya mchezo, huku lile la Altetico lilkiwekwa kamabni na mchezaji Angel Correa katika dakika ya 61 ya mchezo.
Mechi hiyo ilikuwa ngumu n a kushuhudiwa nyota wa klabu ya soka ya Barcelona Lionel Messi akitolewa nje baada ya kuumia katika dakika ya 58 ya mchezo.
Post a Comment