Baada ya klabu ya Simba kulalamika juu ya ubovu wa uwanja hatimaye TFF imekubali ombi lao na kusogeza Mechi mbili za raundi ya sita za Ligi Kuu ya soka Tanzania bara kati ya Simba na Majimaji,kuchezwa kwenye Uwanja wa Taifa badala ya Uwanja wa Uhuru mashabiki wa klabu hiyo wamefurahishwa na kitendo hicho.
wakizungumza na Kilowoko.blogspot.com mashabiki hao wamesema walikuwa wanapata shida wakati wakiishuhudia timu yao hiyo ikiwa inacheza katika uwanja wa Uhuru lakini kwa sasa kwao ni kicheko tu.
Mabadiliko hayo yametokana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kusitisha kwa muda kuutumia Uwanja wa Uhuru katika kipindi hiki ambacho limeanza kufanyia marekebisho sehemu ya uwanja huo ambayo ni ya nyasi bandia (artificial turf).
Hivyo, mchezo wa Simba na Majimaji utachezwaa Jumamosi, Septemba 24 wakati wakati ule wa African Lyon na Kagera Sugar ikichezwa Jumatatu, Septemba 26.
Septemba 25 Uwanja Taifa utatumiwa kwa mechi ya timu za Wabunge za Simba na Yanga ili kuchangia waathirika wa janga la tetemeko lililotokea mkoani Kagera.
Kutokana na marekebisho yanayofanyika Uwanja wa Uhuru, mechi ya kundi ya A ya Ligi Daraja la Kwanza kati ya Ashanti United na Pamba iliyokuwa ichezwe kesho Septemba 23 kwenye uwanja huo sasa itafanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam.
Post a Comment