Shirikisho la riadha nchini RT limethibitisha
kuendelea vyema kwa michuano ya Dar Lottery Marathon ambayo imepangwa kufanyika
jijini Dar es salaam oktoba 14
Kaimu katibu mkuu wa RT Ombeni Zavala amesema
washiriki mbali mbali wameendelea kuthibitisha ushiriki wa michuano hiyo kutoka
ndani nan je ya nchi, huku akisisitiza kwa watanzani wengine wanaohitaji kuwa
sehemu ya michuano hiyo kuendelea kujitokeza bila kusita.
Zavala pia amezungumzia uwezekano wa mtanzania
Alfrence felix Simbu aliyemaliza katika nafasi ya tano kwenye mshike mshike wa
Olimpiki mwaka 2016, kushiriki michuano hiyo ya kimataifa.
Post a Comment