Timu ya soka ya Majimaji FC ya Songea imetangaza
hali ya hatari kwa wekundu wa msimbazi Simba ambao Jumamosi hii watacheza mechi
ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Mjumbe wa kamati ya utendaji ya klabu hiyo Salum Msamaki
amesema wanaamini kikosi chao kitakua cha kwanza kwa msimu huu kuifunga timu ya
Simba ambayo inaongoza msimamo wa ligi ikiwa haijapoteza mchezo hata mmoja kwa
msimu huu wa 2016/17.
Wakati huohuo suala la ukata ndani ya klabu ya
Majimaji FC huenda likafikia kikomo siku kadhaa zijazo, kufuatia neema ya
udhamini inayoinyemelea klabu hiyo kongwe huko mkoani Ruvuma.
Salum Masamaki amesema wamekua na mazungumzo na
kampuni ya GSM ambayo imeonyesha dhamira ya kweli ya kuwekeza ndani ya Majimaji
FC.
Amesema endapo mambo yatakamilishwa kama
wanavyotarajia, kikosi chao kitakua na kila sababu ya kufanya vizuri katika
michezo inayowakabili na huenda wakamaliza kwenye nafasi nzuri katika msimamo
wa ligi kuu msimu huu.
Post a Comment