Baada ya kutoka suluhu ya na klabu ya soka ya
African Lyion katika mchezo wa Ligi kuu soka Tanzania bara mchezo wa mzunguko
wa 5 klabu ya soka ya Toto Afrika ya Jijini Mwanza imejitapa kuwafundisha soka
Maafande wa Ruvu Shooting katika mchezo wao utakaopigwa Jumapili hii katika
uwanja wa Mabatini.
Afisa habari wa klabu hiyo
Kasbeti Japheti amesema kuwa siku zote soka huwa linabadirika na wao kutoka
suluhu katika kipute hicho sio kwamba wameshindwa kurudisha mashambulizi kwa
wapinzani wao hao bali ni mchezo tu wa soka wakati mwingine huwa unabadirika.
Post a Comment