Kocha mkuu wa klabu ya soka ya Arsenal Arsene Wenger
amefunguliwa milango ya kuweza kuchukua nafasi ya kuwa kocha mpya wa timu ya
taifa ya nchini Uingereza baada ya mkataba wake kumalizika mwishoni mwa msimu
huu katika kalabu yake.
Wenger anaweza akakubali ofa hiyo ya kuwa kocha mpya
wa timu hiyo baada ya kumalizana na klabu yake ya sasa ya Arsenal kutokana na
kuwa bado anaifikiria klabu yake hiyo.
Wenger anaangalziwa kuchukua nagasi hiyo baada ya
kocha wa zamani wa timu hiyo Sam Allardyce's kuwa katika tuhuma nzitobaada ya
kuvuja kwa video inayomuonyesha akihujumu mipango ya usajili ya wachezaji wa Uingereza
pamoja na kukisema vibaya chama cha soka nchini Uingereza FA.
Post a Comment