Waziri wa habari,Utamaduni,Sanaa na michezo Mhe.Nape
Nnauye amezidi kusisistiza na kuwaonya wale wote wanaoanza kuhujumu mfumo wa
matumizi ya tiketi za Elekroniki ambao unaanza kutumika rasmi kuanzia Jumamosii
hii katika mechi ya watani wa Jadi klabu ya soka ya Simba na Yanga.
Akizungumza na waandishi wa habari Nape amesema kumekuwa
na watu wanoanza kuhujumu mfumo huo wa tiketi za Elekroniki ambao wanasababisha
kuonekana kama haujakamilika katika uanzaji wake.
Kwa upande mwingine nape ameelezea jinsi mkataba wa
tiketi za Elecktoniki ulivyosainiwa na kuelekezea kuwa tiketi hizo kwa sasa
zinatolewa bure pasipo malipo yoyote yale.
Post a Comment